Chelsea inapania kumsaini Gonzalo Higuain kwa mkopo hadi mwisho wa msimu
huu - japo Juventus ina mpango kumuuza nyota huyo wa Argentina mwenye
umri wa miaka 31. (Telegraph)
Winga wa England Jadon Sancho, 18, ana mpango wa kusalia Borussia
Dortmund licha ya tetesi kuwa huenda akarejea katika ligi ya Premia.
(Mail)
Everton ni miongoni mwa vilabu vinavyo ng'ang'ania
kumsajili mshambuliaji wa Chelsea na timu ya taifa ya Belgium, Michy
Batshuayi baada ya mkataba wake wa kuchezea Valencia kwa mkopo
kukatizwa. (Telegraph)
Crystal Palace na Fulham pia wanawania kumsaini Batshuayi. (Mirror)
Newcastle imeungana na Liverpool katika kinyang'anyiro cha kumsajili kiungo wa kati wa Trabzonspor Abdulkadir Omur.
Kiungo huyo wa miaka 19 amebatizwa jina la 'Turkish Lionel Messi'. (Sun)
Kiungo
wa kati wa Manchester United na Uhispania Juan Mata, 30, amesema hajui
hatima yake ya siku zijazo baada ya kandarasi yake kukamilika mwisho wa
msimu huu. (AS - in Spanish)
No comments:
Post a Comment