Wachezaji watano wameteuliwa kuwania tuzo ya mchezaji bora
wa ligi kuu ya Vodacom kwa msimu wa 2016/2017.
Wachezaji walioteuliwa kuwania kinyang’anyiro hicho ni
Aishi Manula (Azam
Fc)
Haruna Niyonzima (Yanga Sc)
Mohamed Hussein (Simba Sc)
Shiza Kichuya (Simba
SC)
na Simon Msuva (Yanga Sc)
Majina hayo yatapigiwa kura na makocha , makocha wasaidizi
na manahodha wa timu za ligi kuu ya Vodacom pamija na wahariri wa michezo
kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini.
Wahusika watatumiwa fomu maalum za kupiga kura kwenye email
za klabu zao na vyombo husika vya habari. Mwisho wa kupiga kura ni May 23 2017
saa 6 usiku.
Hafla ya utoaji wa tuzo hiyo ambayo unaratibiwa na kamati ya
Ushauri ya Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) itafanyika May
24 mwaka huu kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment