Monday, October 31
TOP 10: Wachezaji wanaolipwa mshahara mkubwa duniani. Gareth Bale hadi nafasi ya tatu(3) & Pogba nafasi ya tano(5)
Staa wa kimataifa wa Wales anayeichezea klabu ya Real Madrid ya Hispania Gareth Bale ameingia katika TOP 3 ya wachezaji wa soka wanaolipwa pesa ndefu zaidi duniani ambapo ameingia katika list hiyo kutokana na mkataba wake mpya na Real Madrid.
Kwa sasa Bale analipwa pound 346,000 kwa wiki ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 900 ambapo katika kipindi cha miaka sita Bale atakuwa kaingiza jumla ya pound milioni 108.
Paul Pogba naye pia ameingia katika Top 5 ya wachezaji wanaolipwa mkwanja mkubwa zaidi. Kutokana na mkanja huu anaolipwa, unamfanya kuwa mchezaji anaelipwa mshahara mkubwu ndani ya club ya Manchester United kuliko mchezaji yeyote ndani ya club hiyo. Kwa sasa Pogba anapokea pound 290,000 kwa wiki, huku Mkongwe Wayne Rooney akipokea pound 260,000 kwa wiki na Zlatan Ibrahimovic anapokea pound 250,000 kwa wiki.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment