Simba SC ilianza mchezo wake wa kwanza hatua ya Makundi ya CAF Champions
League dhidi ya JS Saoura ya Algeria, Simba SC ilikuwa inacheza na
timu ambayo inatajwa kuwa changa katika michuano ya CAF Champions League
lakini uimara wa Simba uliwasaidia kupata matokeo chanya katika game
hiyo.
Simba SC ikiwa na faida ya uwepo wa mashabiki wake uwanjani walifanikiwa kupata ushindi wa magoli 3-0, magoli ya Simba SC yakifungwa na Emmanuel Okwi dakika za nyongeza kabla ya kwenda mapumziko, Meddie Kagere aliongeza magoli mawili dakika ya 51 na 67 na kuifanya Simba SC kutoka kifua mbele katika mchezo huo.
Simba SC sasa itasafiri kwenda Congo January 19 kucheza mchezo wake wa pili dhidi ya AS Vita wakati Al Ahly watakuwa Algeria January 18 kucheza dhidi ya JS Saouro.
No comments:
Post a Comment