Kumbukumbu ya Champions League
- Ole Gunnar Solskjaer ameshindwa kwa
mara ya kwanza kama meneja wa Man Utd katika mechi zote 12 aliyochezwa
chini ya uongozi wake, hii ikiwa pia ndio kipigo kikali walichopewa
nyumbani katika mashindano yoyote ya Ulaya.
- Paris Saint-Germain ni timu ya kwanza
ya Ufaransa kushinda Manchester United katika uwanja wa Old Trafford
katika shindano lolote barani Ulaya kabla ya mechi ya Jumanne usiku).
- Kwanzia mwanzo wa msimu wa mwaka
2016-17, ni Cristiano Ronaldo pekee aliyefunga mabao mengi zaidi
(mabao16) katika mechi za muondoano za Champions league kuliko Kylian
Mbappe wa PSG aliyefunga (mabao 7) kufikia sasa.
- Timu 34 zilizoshindwa mechi ya kwanza
ya muondoano katika Champions League hakuna hata moja iliyofungwa bao
zaidi ya moja nyumbani iliyofanikiwa kuendelea mbele katika juhudi ya
kuwania taji hilo.
- Solskjaer ni meneja wa pili wa
Manchester United kufungwa mechi ya kwanza ya Champions League,baada ya
Louis van Gaal (Ferguson, Moyes and Mourinho wote walishinda).
- Angel Di Maria ameandikisha rekodi ya
kuchangia ufungaji mabao katika Champions League kwa mara ya tatu, na ya
kwanza tangu mwezi Septemba 2013 (wakati wa mechi ya Real Madrid dhidi
ya Galatasaray).
- Gianluigi Buffon amekuwa mchezaji wa
nne kucheza Champions League akiwa na mika 41 (baada ya Marco Ballotta,
Mark Schwarzer na Oleksandr Shovkovskiy); Alishiriki mashaindano hayo
mra ya kwanza kabla ya wachezaji Marcus Rashford na Kylian Mbappe
kuzaliwa.
No comments:
Post a Comment