Legend wa Man United ambaye pia ni mchambuzi wa soka kwa sasa Gary Neville amewataka makocha na viongozi waliopo baada ya kuondoka kwa Jose Mourinho kuhakikisha falsafa ya club hiyo inapewa kipaumbele zaidi ya chochote.
Mourinho ameiongoza Man United kushinda mataji mawili akiwa ameifundisha timu hiyo kwa kipindi cha miaka miwili na nusu, Neville anaamini kuwa club ya Man United anaamini inabidi irudi katika falsafa yake ya kucheza soka la kushambulia na wachezaji wao vijana wawe kiini cha falsafa hizo.
“Hakuna mtu atakayaruhusiwa kuingia katika uwanja wa mazoezi wa Man United au Old Trafford tena kuanzisha falsafa yake mpya, hilo limeisha Man United falsafa ina maana kubwa kama ilivyo kwa FC Barcelona au Ajax, Man United unacheza kwa haraka unacheza soka la kusahmbulia katika njia ya kuburudisha unawaleta wachezaji wachanga unawaamini unawapa nafasi na kushinda”>>>Gary Neville
Kocha wa muda wa Man United Ole Gunnar
No comments:
Post a Comment