Hoteli ya kifahari yashambuliwa Nairobi
Shambulio la Hoteli ya DusitD2 Nairobi Kenya
Polisi wanaendelea na operesheni ya kukabiliana na watu wenye silaha
walioshambulia majengo ya 14 Riverside katika mtaa wa Westland, Nairobi
kunakopatikana hoteli ya DusitD2.
Kundi
la wanamgambo wa Kiislamu la al-Shabab, ambalo awali lilidai kuhusika
katika shambulio la Riverside, Nairobi limetoa idadi ya watua ambao
linadai wameuawa.
Ujumbe kwenye mtandao unaoaunga mkono kundi hilo wa Somali Memo unadai idadi ya waliofariki ni 47.Hata hivyo, hakuna ushahidi wowote uliotolewa kuthibitisha hilo.
Polisi bado hawajatoa taarifa yoyote kuhusu majeruhi au waliofariki.
Waziri
wa Usalama Dkt Fred Matiang'i ameeleza tu kwamba Wakenya wengi na watu
wa mataifa ya nje wameokolewa kutoka kwenye jengo hilo, na kwamba
majengo yote yamedhibitiwa.
No comments:
Post a Comment