Friday, January 18

Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 18.01.2019: Ramsey, Hudson-Odoi, Piatek, Sancho, Higuain, Rashford


Aaron Ramsey ametia saini makubaliano ya awali ya mkataba wa kujiunga na Juventus kutoka Arsenal msimu huu.

Kiungo huyo wa miaka 28 tayari amekamilisha vipimo vya afya na mabingwa hao wa Italia wanaoshiriki ligi ya Serie A, wikendi iliyopita. (Sky Sports)

Ramsey anatarajiwa kutia saini mkataba wa miaka minne wa kitita cha euro milioni 300,000 kwa wiki, ambao utamfanya kuwa mchezaji wa Uingereza anaelipwa vizuri zaidi. (Times)


Chelsea wanajiandaa kumpatia Callum Hudson-Odoi, 18, dili mpya ambayo itagharimu kati ya euro 50,000 kwa wiki - hadi euro 70,000 - katika juhudi ya kumfanya asikubali ofa ya kujiunga na Bayern Munich. (Mail)


Juhudi za West Ham za kutaka kumnunua mshambuliaji wa Genoa na Poland Krzysztof Piatek, 23, zimegonga mwamba huku AC Milan wakijaribu bahati yao. (Mail)

Mkurugenzi wa soka wa klabu ya Borussia Dortmund Michael Zorci nayoshiriki ametoa wito kwa vilabu vya ligi kuu ya England dhidi ya uhamisho wa winga wa zamani wa Manchester City Jadon Sancho, 18. (Mirror)
Chelsea wanapania kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa Argentina Gonzalo Higuain, 31, kutoka Juventus ili wamjumuishe katika kikosi kitakachomenyana na Arsenal Jumamosi hii. (London Evening Standard)

Chelsea pia wanakaribia kukamilisha usajili wa kiungo wa kati wa kimataifa wa Argentina Leandro Paredes, 24 anaechezea Zenit St Petersburg kwa kima cha euro milioni 31. (Express)


Manchester United wako tayari kuongeza malipo ya Marcus Rashford kwa hadi euro 150,000 kwa wiki ili kumzuia kiungo huyo wa miaka 21 asihamie vilabu vyovyote vikuu vya Ulaya msimu huu. (Mirror)

No comments:

Post a Comment