Ni fainali ya kihistoria ya Real Madrid na Juventus leo Jumamosi jijini
Cardiff, Wales huku timu hizo mbili kila moja ikiwa imenyakua ubingwa
wa Ligi Kuu nchini mwake msimu huu.
Real Madrid ina kibarua kigumu cha kutetea taji hilo, kutokana na Juventus iliyo katika kiwango cha juu msimu huu.
Mchezo huo wa fainali unahusisha ushindani kwa makocha, wachezaji pamoja na mfumo ndani ya uwanja.
Makocha Zinedine vs Allegri
Utamu wa fainali hiyo umekolezwa na ushindani wa kocha Zinedine Zidane
ambaye ni chimbuko la klabu hiyo ya Italia. Zidane anapambana ili
kuandika historia kuyakua taji hilo kwa mara ya kwanza tangua achukue
mikoba kuinoa klabu hiyo Januari mwaka jana.
Pia, Kocha Massimiliano Allegri anataka kujihakikishia nafasi ya kuwa
miongoni mwa makocha bora mbele ya wapinzani wao, Real Madrid.
Vita ya Ronaldo vs Buffon
Mtifuano katika fainali hiyo ipo kwa makocha pekee. Mchezaji Christiano
Ronaldo anataka kudhihirisha ubora wake mbele ya kipa wa Juventus,
Gianluigi Buffon.
Kipa Buffon amekuwa mahiri baada ya kuzua hatari nyingi kwenye lango
lake huku akiwa ameokoa michomo 13 kwenye mashindano ya Ligi ya
Mabingwa.
Pia, Ronaldo amejikusanyia mabao matano kabla ya kukutana na kipa huyo kwenye mechi hiyo yenye ushindani.
Miongoni mwa mashuti sita aliyopiga Ronaldo, matano yalizaa mabao na
moja lilitoka nje. Wachezaji hao wote wanawania tuzo ya Ballon d’Or
mwaka huu inayotolewa na Chama cha Soka Ulaya (Uefa) ambao ndiyo
waandaaji wa mashindano hayo makubwa.
Ushindani kwenye mfumo
Kocha Allegri atashusha kikosi chake uwanjani huku akitumia mfumo wa
4-2-3. Mfumo huo amekuwa akipenda kuutumia kutokana na kuamini kwamba
ndiyo umemletea mafanikio makubwa.
Zidane ataingiza timu uwanjani huku akitumia mfumo wa 3-4-3.
No comments:
Post a Comment