Wanasheria nchini Uganda wameamua kuifikisha familia ya Ivan Mahakamani
kwa makosa ya kuzika pesa halali za Jamhuri ya Uganda katika kaburi la
ndugu yao Ivan. Kwa nchi yoyote kitendo hicho hakikubaliki kwani pesa
hizo zingeweza kutumika katika shughuli zingine na kukuza uchumi wa
nchi.
Kitendo hicho kinakuja baada ya marafiki wa Ivan kumwaga mamilioni ya
pesa ndani ya kaburi la Ivan kama njia ya kumuaga rafiki yao aliyekuwa
maarufu kwa matumizi makubwa ya pesa.
Wanasheria wakiongozwa na Tugume Gideon wa Human Rights Defenders
Association Uganda wamesema hawakufurahishwa na kitendo cha RICH GANG
cha kuzika mamilioni ya pesa ndani ya kaburi, na kwa vile ni kinyume cha
sheria,
wameamua kwenda mahakamani kuomba kaburi la Ivan lifukuliwe, pesa
zitolewe zikafanye shughuli nyingine na waliohusika washitakiwe kwa
kuharibu kwa makusudi alama ya taifa.
No comments:
Post a Comment