Saturday, February 9

United inahitaji miaka miwili kushinda EPL

Pogba has enjoyed a significant up-turn in form since Ole Gunnar Solskjaer took over Pogba has enjoyed a significant up-turn in form since Ole Gunnar Solskjaer took over

Meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer amesema kikosi chake kinahitaji miaka miwili kushinda EPL.

Meneja  Solskjaer ametilia shaka uwezekano wa klabu hiyo kushinda kombe la ligi kuu ya Premia msimu huu.

Lakini ameongeza kuwa hakuna haja ya kufanyia marekebisho kikosi chake ili kushinda taji hilo.

United wameshinda mechi 10 kati ya 11 tangu Solskjaer alipochukua nafasi ya Jose Mourinho alifutwa kazi mwezi Disemba mwaka jana.

Manchester United wamepanda hadi nafasi ya nne katika jedwali la ligi ya Premia, wakiwa nyuma ya mahasimu wao Liverpool na Manchester City kwa alama 11.

"Mwaka huu tuko mbali kidigo, bila shaka,"alisema Solskjaer.

Dalot na RashfordInabidi tukimbizane na timu zilizo mbele yetu, hususan City, Liverpool na Tottenham - pia wamekuimarisha mchezo wao.

"miaka miwili' sio muda mrefu, lakini pia sio muda mfupi wa kusema tunaweza kuonesha tofauti kubwa katika maandalizi yetu, na kila kitu."

Manchester United haijashindwa hata mechi moja chini Ole Gunnar Solskjaer tangu mwezi Disemba
Raia huyo wa Norway wa miaka 45 ambaye alishinda Tuzo ya meneja wa mwezi wa ligi ya England mwezi Januari tayari ana ''taswira'' ya jinsi "Hii timu ya Manchester United itakavyo kuwa katika kipinda cha miaka michache", hata kama hatapewakazi ya kudumu.

Alipoulizwa klabu hiyo inahitaji wachezaji wangapi ili kushinda taji hilo, Solskjaer alisema: "inategemea pia utendakazi wa wachezaji waliopo kwa sasa.

Ikiwa kila mchezaji anaweza kuboresha mchezo wake kwa kati ya 1-2% na wala sio idadi ya wachezaji.


"Kununua wachezaji nyota pekee haitoshi, tulibadilisha mambo mawili matatu na ghafla tumefikia nafasi ambayo ni rahisi kushinda taji."

 "Nimetoka Molde, walikuwa nafasi ya 10 mwaka 2010, na mwaka 2011 tulishinda ligi, kwa hivyo hatuwezi kusema hilo haliwezekani," alisema.

No comments:

Post a Comment