Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania CHADEMA, Freeman
Mbowe amefutiwa dhamana na mahakama ya hakimu mkazi kisutu mara baada
ya kukiuka masharti aliyopewa.
Maamuzi hayo yametolewa leo kwa madai kuwa alidharau maamuzi ya mahakama.
Na sababu zilizotolewa kudaiwa kuwa hazina ukweli wowote.
Sababu
zilizotolewa ni kwamba Mbowe alishindwa kuhudhuria mahakamani tarehe 8
November 2018 baada ya kuugua ghafla na kwenda Afrika kusini kwa
matibabu.
Mwezi Oktoba 28,alielekea Washing DC Marekani kuhudhuria mkutano na aliporejea tarehe 31 Oktoba aliugua ghafla.
Wakati huohuo mbunge wa Tarime mjini, Esther Matiko pia alifutiwa dhamana wa kukiuka masharti.
Matiku
alishindwa kuhudhuria mahakamani baada ya kwenda kwenye ziara ya
wabunge nchini Burundi, sababu ambayo alielezwa kwamba haikidhi matakwa
ya kushindwa kufika mahakamani.
Mbowe alishtakiwa katika mahakama ya Kisutu pamoja na viongozi wengine
kwa kufanya maandamano kabla ya kufanyika uchaguzi wa eneo bunge la
Kinondoni kinyume na sheria, hatua iliowalazimu maafisa wa polisi kupiga
risasi juu ili kuwatawanya waandamanji.
Utaratibu wa Dhamana ukoje?
Betty Masanja,
Mwanasheria na mchambuzi wa masuala ya jamii anasema kwamba dhamana huwa
ni haki ya kila mtuhumiwa kama kesi yake sio ya mauaji.
Lakini kwa kawaida dhamana huwa inafutwa baada ya mtu kukiuka masharti.
Kuna aina mbalimbali za dhamana na masharti yake huwa yanategemea na kesi yenyewe.
"Kuna mtu akipewa dhamana anaweza kunyang'anywa hati yake ya
kusafiria au anaweza kuachwa nayo lakini hawezi kusafiri mpaka apewe
ruhusa na mahakama.
Kuacha kuhudhuria mahakamani kwa mshakiwa bila
sababu au sababu yake kutokubaliwa na mahakama kunaweza kupelekea
dhamana kufutwa" Masanja aliiambia BBC.
Kufutiwa dhamana kuna maana gani?
Mtu
akifutiwa dhamana hii ina maana kwama mtuhumiwa atatakiwa kukaa mahabusu
ili aweze aweze kuhudhuria mahakamani kama anavyohitajika bila
vipingamizi vyovyote.
Mtu akifutiwa dhamana anaweza kupata dhamana
kwa mara nyingine mpaka wakili wake aandike sababu za kisheria kwa
mahakama na kueleza sababu za kwa nini asifutiwe na kwa nini aendelee
kubaki uraiani?
No comments:
Post a Comment