Baada ya kucheza mchezo wao wa kwanza nyumbani wa hatua ya Makundi wa
CAF Champions League, Simba SC ilifuata kwa kucheza michezo yao ya pili
ya michuano ugenini, baada ya kupoteza 5-0 dhidi ya AS Vita katika jiji
la Kinshasa DRC, Simba jana ilikuwa Alexandria Misri kukipiga dhidi ya
Al Ahly.
Simba ambao walikuwa na jeraha la kupoteza kwa magoli 5-0 mchezo wao
wa AS Vita, walijikuta wakiingia kwenye aibu nyingine tena baada ya
kujikuta wakipokea kipigo kingine cha magoli 5-0, huku Al Ahly ikimkosa
nyota wake Ramadan Sobhi kwa majeraha.
Dakika 45 za kwanza za mchezo Simba walijikuta wakiwa wameruhusu tayari magoli
5-0, hivyo baada ya kuongeza nidhamu ya ulinzi kipindi cha pili,
walifanikiwa kuzuia na kutoongezwa goli lolote, kipigo hicho kinaifanya
Simba iendele kuwa nafasi ya tatu kwa kuwa na point 3, JS Saoura
akishika mkia kwa kuwa na point 2.
Magoli ya Al Ahly yalifungwa na Sulaya dakika ya 3, Maaloul dakika ya
23, Ajayi dakika ya 31 na Walid aliyefunga magoli mawili dakika ya 34 na
40, baada ya game hiyo Simba sasa watacheza game yao ya nne nyumbani
dhidi ya hao hao Al Ahly February 12 2019 uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment