Teknolojia ya VAR au ya kutumia video kutoa uamuzi itaanza kutumika katika ligi kuu ya England msimu ujao baada ya vilabu vinavoshiriki ligi hiyo kukubaliana kimsingi.
Tayari majaribio yamekuwa yakifanywa katika baadhi ya mechi za msimu huu.
Wasimamizi wa mechi za ligi hiyo wanatarajiwa kutuma ombi rasmi kwa bodi ya kimataifa ya kandanda na shirikisho la kandanda duniani FIFA.
Tayari teknolijia hiyo inatumika katika ligi za Italia na Ujerumani ili kutoa uamuzi.
No comments:
Post a Comment