Mwimbaji wa Bongo Fleva Nedy Music
ambaye pia yupo chini ya record label ya PKP ameshinda tuzo ya ‘African
Fans Favourite” katika tuzo za AFRIMMA zilizofanyika November 24 2018
Ghana.
Nedy Music ametumia ukurasa wake wa
Instagram kuwashukuru wale wote waliompigia kura ikiwa pamoja na wimbo
uliomfanya apate tuzo hiyo “One and Only” aliomshirikisha Ruby.
Neddy Music ameandika >>> “Asante
Mungu Safari hii imekuwa kubwa na yenye matunda sana kwangu .
Ninamshukuru Mungu, familia yangu, timu yangu na Mashabiki wangu wote
ndani na nje kwa kunisapoti hasa kijana wenu katika kazi yangu ya muziki
na Kuhakikisha nasukuma gurudumu la muziki mbele zaidi”
“Bila kusahau Vyombo vyote vya Habari
Tanzania na duniani kote, yote ilianza kama ndoto lakini kujiamini kwa
kile nilichokua nafanya kwa bidii na kuzingatia kile nilichokua nataka
mbeleni ingali bado safar ni ndefu kwangu….sisemi haya kwa kujisifu
lakini kuwa mshindi kwenye tuzo kubwa kama hii ambazo zinaunganisha
mataifa 52 Ni kubwa sana kwangu na Nchi yangu pia ”
“Mashabiki
wangu wote na wapenda burudani ambao hamkuchoka kupiga kura kila sku
Asanteni sana sana, Naomba mzidi kunisapot nami nawaahidi
kutowaangusha… Kubwa Zangu Shukran kwa My Brother @ommydimpoz Kwa Jinsi ulivyonishika na kunisaidia kusogeza hatua yangu sitaacha kutoa shukran zangu kwako”
“Kila hatua ntayoendelea nayo kwangu Pia Producer wa Wimbo uliopelekea kuwa kwenye kinyang’anyiro @yogobeats na msanii nilieshiriki nae fika @iamrubyafrica Bila kumsahau Bwana Director @hanscana_ Thanks @afrimawards for this award “African fan’s favourite "
No comments:
Post a Comment