Monday, May 15

Mkoa wa Geita unahitaji wauguzi zaidi ya 1000







Mkoa wa Geita unahitaji waaguzi zaidi ya elfu moja na mia mbili  ambapo kwa sasa waliopo ni zaidi mia saba hamsini, wauguzi hao wanahitajika haraka ili kumaliza tatizo hilo na kuwawezesha wauguzi waliopo kufanya kazi zao kwa weledi bila kulemewa na wagonjwa.

Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya waaguzi duniani wilayani Mbogwe Mwenyekiti wa chama cha wauguzi Mkoani Geita Amina Ng'ombo amesema uhaba huo una wafanya wauguzi pamoja na madaktari kutopata muda wa mapumziko.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Geita Dk Joseph Kisala amekiri kuna ukosefu wa wauguzi Mkoani humo.
Nae Mwenyekiti wa chama cha wauguzi Mkoani Geita Amina Ng'ombo amesema wana upungufu wa wauguzi ambapo muuguzi mmoja anahudumia wagonjwa mia moja

Kauli mbiu ya siku ya maadhimisho ya wauguzi duniani ni uuguzi ni sauti inayoongoza katika kufikia malengo endelevu ya maendeleo.

No comments:

Post a Comment